Mbulu dc
Ukurasa rasmi wa Halmashauri ya Wilaya ya mbulu
09/08/2026
HABARI PICHA
Matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea Agosti 8,2026 katika Maonyesho ya 32 ya Nanenane kanda ya Kaskazini kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Manyara Rs
Michael Semindu
Abubakar Kuuli
09/08/2026
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Abubakar Kuuli leo Agosti 9,2026 ameshiriki jogging maalumu ikiwa ni hamasa kwa wananchi kuelekea tukio kubwa la Manyara Tanzanite Marathon litakalofanyika mnamo Agosti 22,2026.
Jogging hiyo Maalum imeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi.
Manyara Rs
Manyara Tanzanite Marathon
Abubakar Kuuli
08/08/2026
MBULU DC YANG’ARA MAONYESHO YA NANE NANE, YASHINDA TUZO TATU KWA MPIGO
Na Magreth Mbawala,Mbulu DC
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imekuwa miongoni mwa Halmashauri zilizong’ara zaidi katika Maonyesho ya 32 ya Nane Nane Kanda ya Kaskazini baada ya kunyakua tuzo tatu kwa mpigo.
Tuzo hizo zimetolewa leo, Agosti 8, 2026, wakati wa kufungwa kwa Maonyesho ya 32 ya Nane Nane Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika Viwanja vya Themi-Njiro, jijini Arusha.
Tuzo zilizopatikana ni pamoja na Mshindi wa Pili katika Mazao ya Kilimo, Mshindi wa Kwanza katika Ufugaji wa Ng’ombe wa Maziwa, pamoja na Mshindi wa Kwanza kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu katika Sekta ya Kilimo.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hizo, Mkuu wa Idara ya Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Elifadhili Manahiri, amesema ushindi huo umetokana na juhudi za wakulima na wafugaji kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo na mifugo wanaotoa elimu na ushauri wa kitaalamu.
Amesema ushindi huo umeipa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu heshima kubwa, huku ukiwa chachu ya kuwahamasisha wakulima na wafugaji kuongeza juhudi katika uzalishaji na kutumia mbinu bora za kilimo na ufugaji.
Aidha, ushindi huo unatarajiwa kuhamasisha wakulima na wafugaji wengine kutumia mbegu bora, kuzingatia lishe bora ya mifugo na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza tija na uzalishaji.
Katika hafla hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imepokea zawadi mbalimbali ikiwemo makombe, vyeti pamoja na hundi za fedha.
Manyara Rs
OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI
Michael Semindu
Maelezo News
08/08/2026
RC MAKALA AWATAKA WAKULIMA KANDA YA KASKAZINI KUACHA KILIMO CHA MAZOEA
Na Magreth Mbawala,Mbulu DC
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA.Amos Makala leo Agosti 8,2026 amefunga rasmi maonyesho ya 32 ya Nane Nane Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha maonesho ya 32 ya Nanenane kanda ya kaskazini Mhe.Makala amewataka wakulima kuacha kilimo cha mazoea na kuanza kutumia kilimo cha kisasa chenye tija na ushindani sokoni.
Pia amewataka wakulima kujikita kwenye Kilimo cha umwagiliaji,ufugaji wa kisasa,uvunaji wa maji ya mvua,upandaji wa malisho kwa mifugo pamoja na kupanda mazao yanayostahimili ukame.
“Wakulima tumieni tafiti mbalimbali zinazofanywa na wataalamu ili kujua kalenda za kilimo pamoja na mbegu bora.”Amesema Mhe.Makala.
Sambamba na hilo Mhe.Makala ametoa rai kwa maafisa ugani kutoa elimu sahihi na kuwafata wakulima mashambani kwani wao ni daraja kati ya Serikali na Wananchi.
Aidha,Mhe.Makala alisema Serikali ya awamu ya sita imefanya kazi kubwa kwenye sekta ya Kilimo kwa kuongeza thamani ya bei za mazao,kuboresha huduma za kilimo na vitendea kazi.
Akihitimisha hotuba yake Mhe.Makala alisema Maonyesho ya Nanenane Mwakani yataambatana na AFCON hivyo wakulima wajiandae vyema kutumia fursa hiyo.
Manyara Rs
OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI
Maelezo News
Michael Semindu
08/08/2026
Heri ya Sikukuu ya Nanenane
Manyara Rs
Abubakar Kuuli
Wizara ya Kilimo
07/08/2026
Watumishi karibuni Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu,Tunawatakia utumishi uliotukuka.
KwaPamoja Tunaijenga Mbulu Yetu.
Manyara Rs
Maelezo News
OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI
Michael Semindu
Abubakar Kuuli
06/08/2026
DC SEMINDU AHAMASISHA USHIRIKI WA WATUMISHI KATIKA MANYARA TANZANITE MARATHON
Na Magreth Mbawala,Mbulu DC.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe.Michael Semindu leo Agosti 6,2026 amekutana na makundi mbalimbali ya Watumishi wa umma na kuwataka washiriki kikamilifu katika mbio za Manyara Tanzanite Marathon zinazotarajia kufanyika hivi karibuni Mkoani Manyara.
Akizingumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu,DC Semindu alisema mbio hizo ni fursa muhimu si tu kukuza afya bali pia ni chachu ya kuutangaza utalii ndani ya Mkoa wa Manyara.
Aidha,alisema fedha zitakazopatikana kutokana na mbio hizo zitasaidia kuchangia ujenzi wa jengo maalum la huduma za watoto wachanga na njiti pamoja na kununua vifaa tiba kwenye hospital zote za Wilaya ndani ya Mkoa wa Manyara.
Sambamba na hilo aliwataka Watendaji wote kwenda kuhamashisha Wananchi kupitia mikutano, matangazo ya sauti na mbao za matangazo ili wajitokeze kujisajili kwa ajili ya kushiriki mbio hizo.
Mwisho Manyara Tanzanite inatarajia kufanyika mnamo Agosti 22,2026 kwenye viwanja vya Tanzanite Kwaraa Babati Mjini.Mazoezi kwa ajili ya kujiandaa ni kila mbio hizo ni kila Jumamosi saa 12 Asubuhi.
Kauli mbiu kweye mbio hizo ni “Hatua Moja,Okoa Maisha ya Mtoto.”
Manyara Rs
Queen Cuthbert Sendiga
Michael Semindu
Abubakar Kuuli
06/08/2026
MHE.AWESO ASISITIZA UMUHIMU KUTUNZA AMANI MBULU
Waziri wa Maji,Mhe.Jumaa Aweso amesisitiza wananchi kutunza amani na kupinga viashiria vyovyote vya vurugu na kuacha kufata mkumbo wa watu wanaotaka kuvunja amani.
Hayo yamesema Agosti 5,2026 wakati akifanya ziara ya kikazi Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo Mhe.Aweso ni mlezi wa Mkoa wa Manyara.
Akizungumza na Wananchi Mhe.Aweso aliwataka kuepuka uvunjifu wa amani kwani madhara yake yanaathiri watu wote bila kujali umri.
“Kuvunja amani ni k**a hewa ya Oksijeni ikikosekana kwenye anga inaathiri wote wakubwa kwa wadogo,wenye nacho na wasionacho.”Alisema Mhe.Aweso
Pia aliendelea kusema ili maendeleo yaweze kufika kwa wakati na kwa ukubwa ni lazima kuwepo na amani na utulivu.Alisema kuwa bila amani na utulivu maendeleo yanachelewa na rasilimali zinatumika vibaya.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu alisema yeye k**a Mwenyekiti wa ulinzi na usalama atahakikisha amani inaendelea kutunzwa Wilayani kwake.
Akimalizia hotuba yake Mhe.Aweso alimpongeza Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini Mhe.Dkt.Emanuel Nuwas kwa uchapakazi wake na kuwasemea wananchi wa Mbulu Vijijini na kuhakikisha maendeleo yanafika Mbulu Vijijini.
Manyara Rs
Wizara ya Maji/Ministry of Water - Tanzania
Michael Semindu
Abubakar Kuuli
05/08/2026
WAZIRI AWESO AWATAKA WATENDAJI MBULU KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UWAZI
Na Magreth Mbawala,Mbulu DC
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, ambaye pia ni Mlezi wa Mkoa wa Manyara, amewataka watendaji wote wa Serikali kufanya kazi kwa bidii na uwazi ili kuendelea kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali yao.
Wito huo ameutoa leo, Agosti 5, 2026, wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na kukutana na watendaji wa Serikali.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Aweso alisisitiza kuwa kila mtendaji anapaswa kutekeleza majukumu yake kwa bidii katika eneo lake ili kuendelea kutoa huduma bora na kuleta maendeleo kwa wananchi.
“Haipendezi changamoto zilizo ndani ya uwezo wenu kuja kutatuliwa na viongozi au Waziri kutoka Dodoma,” alisema Mhe. Aweso.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Michael Semindu, alimpongeza Mhe. Aweso kwa kuwa kiongozi msikivu na mchapakazi na kufanya vizuri kwenye Wizara ya Maji.
“Wilaya ya Mbulu maji yanatoka, na katika maeneo mengi huduma ya maji imefika. Hata Mbulu Vijijini wananchi wanapata maji kwa kutumia kadi za malipo ya kabla,” alisema Mhe. Semindu.
Naye Mbunge wa Mbulu Vijijini, Mhe. Dkt. Emanuel Nuwas, alimshukuru Mhe. Aweso kwa kutembelea jimbo lake na kumuomba amfikishie salamu Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Mbulu Vijijini.
Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Aweso alimpongeza Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wengine kwa ushirikiano mkubwa uliopo wilayani hapa.
Manyara Rs
Wizara ya Maji/Ministry of Water - Tanzania
Michael Semindu
Abubakar Kuuli
05/08/2026
MRADI WA SHULE WA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 330 WAZINDULIWA MBULU DC
Na Magreth Mbawala,Mbulu DC
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, leo Agosti 5, 2026, amezindua na kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Awali na Msingi iliyopo ndani ya eneo la Shule ya Sekondari Dinamu.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi, Mhe. Aweso alisema ameshangazwa na uwepo wa Shule ya Msingi na Sekondari katika eneo moja, jambo ambalo hata jimboni kwake bado halipo.
Aidha, Mhe. Aweso alisifu ubora wa majengo ya shule hiyo na kusema kuwa hayana tofauti na yale ya shule binafsi.
“Mheshimiwa Rais ameweka mazingira mazuri na sahihi ya kujifunzia. Anataka watoto wetu wapate elimu bora inayoleta tija katika ulimwengu wa sasa,” alisema Mhe. Aweso.
Sambamba na hilo, Mhe. Aweso aliwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii, akieleza kuwa tayari wana mazingira mazuri ya kujifunzia na kwamba elimu ndiyo itakayomwezesha mtoto wa mfugaji kuwa daktari bingwa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Michael Semindu, alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuleta miradi ya maendeleo, kuboresha miundombinu na kuleta ajira mpya ndani ya Wilaya ya Mbulu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Mhe. Dkt. Emanuel Nuwas, alimshukuru Mhe. Aweso kwa kutembelea jimbo hilo na kujionea kwa macho kazi kubwa zinazofanywa na Serikali.
Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Aweso alimpongeza Mhe. Semindu pamoja na watendaji wote wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.
rs
Wizara ya Maji/Ministry of Water - Tanzania
Msemaji Mkuu wa Serikali
Michael Semindu
Abubakar Kuuli
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the organization
Telephone
Website
Address
Mbulu
Manyara
Opening Hours
| Monday | 09:00 - 17:00 |
| Tuesday | 09:00 - 17:00 |
| Wednesday | 09:00 - 17:00 |
| Thursday | 09:00 - 17:00 |
| Friday | 09:00 - 17:00 |
Alerts
Be the first to know and let us send you an email when Mbulu dc posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.