CG FM Radio
πCG FM RADIO
π88. 5 MHz
πTabora - Tanzania
π+255769354641
πCG Online Tv Owned by C.G. Throughout its existence it has never been involved in any legal wrangle.
Traders, the C.G fm Radio Station started broadcasting services in Tabora municipality in 2004 after being registered by the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) on September 1, 2004. The Radio Station has built a good working relations at high level of integrity with many residents of Tabora region and other audiences in the neighbouring regions of Singida, Shinyanga and Kigoma regions. On top of that it has good working relations with government leaders, policy makers, religious leaders, Civic Organisations, Community Based Organisations (CBOs), Faith Based Organisations (FBOs), Small and Medium Enterprises (SMEs) and other actors in the media arena
The Radio Station has ample potentials for growth and expansion of services in the forthcoming years, because is well prepared in terms of coping with the the latest transmission technology in Tanzania.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 70, Mwanaisha Saidi Juma, mkazi wa Kitongoji cha Madibira, Kata ya Magugu wilayani Babati, Mkoa wa Manyara, amefariki dunia usiku wa kuamkia Oktoba 16, 2026, baada ya kujinyonga huku chanzo cha uamuzi huo kikiwa bado hakijafahamika.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea wakati familia ikiwa kwenye maandalizi ya mwisho ya harusi ya mtoto wake wa mwisho wa kiume iliyopangwa kufanyika Oktoba 17, 2026.
Mtoto wa marehemu, Sadik Musa, ameeleza kuwa hakukuwa na changamoto wala tatizo lolote lililokuwa likimkabili mama yao wakati wa maandalizi hayo ambalo lingeweza kumsababishia msongo wa mawazo.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Omary Rajab, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku uchunguzi wa Jeshi la Polisi ukithibitisha kuwa kifo chake kilitokana na kukosa hewa baada ya kujinyonga.
16/10/2026
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamsaka Athumani Mbuti, mkazi wa Kijiji cha Mvule, Wilaya ya Same, kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Abubaswati Shaban Mbawala, mwenye umri wa miaka 26.
Tukio hilo limetokea Oktoba 15, 2026, katika Kitongoji cha Mapalakang'a, Kijiji cha Mvule, Kata ya Kihurio, Wilaya ya Same, ambapo marehemu alikutwa amefariki dunia akiwa na majeraha mwilini.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo, mtuhumiwa anadaiwa kutoweka pamoja na familia yake na mifugo aliyokuwa akifuga nyumbani kwake.
Jeshi la Polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa huyo ili aweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi limewataka wananchi wenye taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa mtuhumiwa huyo kuzifikisha katika kituo cha polisi kilicho karibu au kutumia njia rasmi za mawasiliano za jeshi hilo.
16/10/2026
Mkandarasi anayetekeleza Mradi
wa Maji wa Miji 28 Kayanga, Karagwe ametakiwa kuhakikisha Disemba 2026 wananchi wa Karagwe wapate huduma ya maji.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) ametoa maelekezo hayo wakati akikagua utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa na mkandarasi AFCON infrastructure limited na Vijera projects and infrastructure limited kutoka India.
"Mara yangu ya mwisho kufika hapa maendeleo ya mradi hayakua mazuri, ila leo niwapongeze mmefanya kazi nzuri na mradi upo katika hatua nzuri, sasa niwaagize Hadi Disemba 2026 mradi uanze kutoa huduma," Mhandisi Kundo amesema
Mradi wa Maji wa Miji 28 kutoka chanzo cha maji cha ziwa Rwakajunju utekelezaji umefika asilimia 79.82 na thamani ya kiasi cha shilingi bilioni 64.32 utaondoka changamoto ya maji kwa wakazi wapatao 352,790 katika mji wa Kayanga na vijiji 29 vya wilaya ya Karagwe kwa kuwezesha huduma ya maji kuwa asilimia 100 kutoka asilimia 65 ya sasa.
Watu wasiofahamika wamevunja, kuharibu na kuiba nyaya za umeme zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja katika nyumba ambayo bado inaendelea na ujenzi, iliyopo eneo la Inala Cheyo, Manispaa ya Tabora.
Akizungumza katika eneo la tukio, mwenye nyumba hiyo, Sauda Juma, mkazi wa Ipuli, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 15, kati ya saa 9 na saa 10 alasiri, baada ya kuondoka katika eneo hilo la ujenzi.
Amesema watu hao walivunja mlango wa mbele wa nyumba hiyo, kuharibu mfumo mzima wa umeme na kuondoka na nyaya pamoja na baadhi ya vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na kijana wake aliyekuwa akilala katika nyumba hiyo nyakati za usiku.
Sauda amesema tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya wizi katika eneo hilo, akieleza kuwa baadhi ya majirani zake wanaojenga nyumba wamekuwa wakiibiwa vifaa mbalimbali, ikiwemo madirisha ya vyoo na grill, hali inayowarudisha nyuma katika harakati zao za ujenzi.
Kutokana na hali hiyo, ameiomba serikali ya mtaa kuanzisha programu ya ulinzi shirikishi itakayowezesha wakazi kushirikiana katika kulinda mali zao na kudhibiti vitendo vya uhalifu katika eneo hilo.
Usikose Kuungana Nasi Katika Taarifa Yetu ya Habari Ifikapo Saa 10:00 Jioni leo, October 16, 2026.
1. Kijana mmoja anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 amenusurika kufa baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya umeme kata ya Itetemia halmashauri ya manispaa ya Tabora
2. Kimataifa Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Gutteresh ametoa wito wa matumizi ya ubunifu wa na teknolojia kwenye uwekezaji wa chakula.
Sikiliza Kupitia: 88.5 MHz | Sauti ya Mamlaka,π» YouTube: .
Usipitwe na Taarifa ya Ifikapo saa Kumi Jioni
Endelea Kutufuatilia kwenye Mitandao yetu ya Kijamii Instagram,Facebook,Tiktok na Youtube na Sikiliza CG Fm 88.5Mhz.
Aliyedaiwa Kumuua Mkewe kwa Risasi Afikishwa Kortini | Moring Power | October 16.
16/10/2026
Miss Grand International imeweka hadharani rekodi ya watazamaji katika mashindano ya mwaka 2026, huku mshindi wa taji hilo, Mtanzania Jihan Mohin Dimachk, akitajwa kuwa sehemu ya historia hiyo.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, kuanzia Septemba 18 hadi Oktoba 16, 2026, maudhui ya mashindano hayo yalifikisha jumla ya watazamaji bilioni 2.33 kupitia mitandao minne ya kijamii.
Takwimu zinaonesha kuwa Instagram iliongoza kwa kutazamwa mara bilioni 1.4, ikifuatiwa na TikTok yenye watazamaji milioni 581.7, Facebook milioni 334 na YouTube milioni 22.5.
Ushindi wa Jihan Dimachk umeendelea kuiweka Tanzania katika jukwaa la kimataifa la mashindano ya urembo, huku rekodi hiyo ikionesha ukubwa wa mwitikio wa mashabiki wa mashindano hayo kwenye mitandao ya kijamii.
Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18, ambaye jina lake halikufahamika mara moja, amenusurika kifo baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya umeme katika Kitongoji cha Kwihala, Kata ya Itetemia, Manispaa ya Tabora.
Akizungumza na CG FM Radio, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kwihala, Tito Stephano, amesema wananchi walikuwa katika harakati za kumchoma moto kijana huyo kabla ya serikali ya kitongoji kuingilia kati na kuzuia mpango huo.
Stephano amesema siku ya tukio kijana huyo alivamia nyumba ambayo bado haikamilika na kuanza kuiba nyaya na vifaa vya umeme vilivyotumika kufanya wiring katika nyumba hiyo kabla ya majirani kmuona na kuanza kumshambulia kwa sialaha za jadi na kumvunja mkono.
Katika mahojiano ya awali kijana huyo alidai kutumwa kufanya uhalifu huo na fundi aliyefanya wiring katika nyumba hiyo.
Baadae jeshi la polisi lilifika na kuondoka na mtuhumiwa huyo.
15/10/2026
Bodi ya Tumbaku Tanzania imeweka mikakati ya kuboresha usimamizi wa masoko ya tumbaku kwa msimu wa 2026/2027, ikiwemo kutoa elimu kwa wakulima kuhusu mwenendo wa soko la dunia na umuhimu wa kuzalisha tumbaku yenye ubora.
Mikakati hiyo imewekwa katika kikao kazi kilichofanyika jijini Mwanza, kilicholenga kutathmini changamoto za msimu wa 2025/2026 na kuimarisha maandalizi ya msimu mpya.
Akiongoza kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Stanley Mnozya, amewataka watumishi kusimamia masoko kwa weledi, uadilifu na haki kwa wakulima na wanunuzi.
Mnozya amesema takribani kilo milioni 190 za tumbaku zilinunuliwa katika msimu uliopita, huku akieleza kuwa bei ya wastani iliyokubaliwa kwa msimu wa 2026/2027 ni dola za Marekani 2.05 kwa kilo, kutegemea madaraja ya ubora na masharti ya soko.
Mnozya amewataka wakulima kuanza maandalizi ya mashamba mapema, kutumia pembejeo kwa usahihi, kusimamia ubora kuanzia vitaluni hadi ukaushaji na upangaji wa madaraja, pamoja na kudhibiti gharama za uzalishaji ili kuongeza tija na kuboresha mapato yao.
15/10/2026
Watu wasiopungua 28, wakiwemo wanafunzi 27 na mwalimu mmoja, wamefariki dunia baada ya paa la shule kuporomoka katika mji wa Peshawar, nchini Pakistan.
Msemaji wa Hospitali ya Lady Reading, Mohammad Asim, ameiambia BBC kuwa watu wengine 19 wamejeruhiwa katika tukio hilo, huku watano wakiwa katika hali mahututi na kuongeza kuwa watoto wengi wamepata majeraha ya kichwani.
Wakati huo huo, wazazi wengi wamewasili hospitalini kufuatilia hali za watoto wao, huku uongozi wa hospitali ukiomba msaada wa polisi kudhibiti umati wa watu.
Kwa mujibu wa msemaji huyo, wanafunzi walioathiriwa na tukio hilo wana umri wa kati ya miaka sita na 12.
Jina la shule hiyo bado halijatolewa rasmi, na majina ya mwalimu pamoja na wanafunzi waliofariki hayajatangazwa hadharani.
Maafisa wa uokoaji wanahofia kuwa huenda kuna watoto na watu wengine waliokwama chini ya vifusi, hivyo idadi ya vifo inaweza kuongezeka kadiri shughuli za uokoaji zinavyoendelea.
Hadi sasa, chanzo cha kuporomoka kwa paa hilo hakijafahamika.
Naibu Waziri Mkuu wa Pakistan, Ishaq Dar, katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, ametoa pole na rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, huku akisema Waziri Mkuu na Serikali wamepokea kwa uzito mkubwa taarifa za tukio hilo.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
PO Box 2207 TABORA
Tabora
Alerts
Be the first to know and let us send you an email when CG FM Radio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.